Articles by "Kimataifa"

http://www.cefc.com.hk/wp-content/uploads/2015/01/communication_sin300_37118315.jpg

Rais wa China Xi Jinping ametaka kuwepo uvumilivu kutoka pande zote wakati wa mawasiliano ya simu na rais wa Marekani Donald Trump siku moja baada ya Korea kusema kuwa ilikuwa tayari kuzamisha meli ya kubeba ndege za vita ya Marekani.
Mawasiliano hayo ya simu ndiyo ya pili kati ya viongozi hao wawili tangu wakutane huko Florida mapema mwezi huu.
Ni ishara ya hofu ya China kuwa msukosuko kati ya Marekani na Korea Kaskazini utasababisha mzozo.
Siku ya Jumapili vyombo vya habari nchini Korea Kaskazini vilisema kuwa jeshi la Korea Kaskazini lilikuwa tayari kuzamisha meli ya Marekani ya USS Carl Vinson, ambayo Marekani inasema itawasili katika rasi ya Korea siku chache zinazokuja.
Meli hiyo ilitumwa na Rais Trump huku onyo ikitolewa kuwa Marekani imepotza uvumilivu kwa mipango ya nuklia ya Korea Kaskazini.
Wakati wa mazungumzo hayo ya simu Bwana Xi alitaka pande zote kuwa wavumulivu na kuzuia vitendo ambavyo vimaweza kuzua mzozo.
Ikulu ya White House inasema kuwa bwana Trump amesisitiza kuwa vitendo vya Korea Kaskazini vinavuruga rasi wa Korea.
 Viongozi hao walikutana kati ya tarehe 7 na 8 huko Florida na baada kuzungumza kwa njia ya simu kuhusu Korea Kaskazni tarehe 12 mwezi Aprili.
source; bbc/swahili

Bingwa wa kutoa motisha afariki Afrika Kusini

Afrika Kusini inaomboleza kifo cha Ontlametse Phalatse, msichana wa umri wa miaka 18 ambaye alikuwa anaishi na ugojwa unaojulikana kama Progeria, ambayo ni hali ya kimaumbile isiyo ya kawaida ambayo husababisha mtu kuzeeka kwa haraka.
Mwezi uliopita Ontlametse alisherehekea siku ya kuzaliwa na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.
Seriklia ya Afrika kuisni imeongoza taifa kutuma rambi rambi kufuatia kifo hicho.
Alifariki hiyo jana katika hospitali ya Dr George Mukhari Academic iliyo nje ya mji wa Pretora.
Phalatse alikuwa mmoja wa wasichana wawili waliokuwa na hali hiyo nchini Afrika Kusini.
Alijiita "mama wa kwanza" , baada ya kuwa mtoto wa kwanza mweusi nchini Afrika Kusini, kupatikana akiwa na ugonjwa wa Progeria.
Alitajwa kuwa mtoto wa kuwapa watu motisha na mtot wa miujiza baada ya kuishi kuliko matarajio walioyokuwa nayo madaktari waliosema kuwa angefariki miaka minne iliyopita.
Rais Zuma ametuma rambi rambi zake kwa familia ya msichana huyo.
Bingwa wa kutoa motisha afariki Afrika Kusini
source:www.bbc.com/swahil

Image result for marijuana


Uruguay itaanza kuuza bangi kwenye maduka ya dawa kuanzia Julai.Nchi hiyo ya Marekani Kusini itakuwa ya kwanza duniani kuuza Bangi kihalali kwa matumizi ya kujiburudisha tu.
Safari ya kuhalalisha matumizi ya bangi ilianza mwaka wa 2013 baada ya sheria iliyokubali uuzaji na ununuzi wake kupitishwa.
Hata hivyo imechukua muda mrefu kwa sheria hiyo kuanza kutumika.
"Bangi itauzwa kwenye maduka ya dawa kuanzia Julai," msaidizi wa Rais, Juan Andre Roballo alisema katika kikao na wanahabari.
Sheria hii inawataka wanunuzi kujisajili na serikali. Bei yake itakuwa $1.30 kwa gramu moja.
Watakaojisajiliwa lazima wawe raia wa Uruguay au wakazi wa kudumu wa nchi hiyo na hawaruhusiwi kununua zaidi ya gramu 40 kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Marijuana hiyo itakuwa inapandwa kwenye mashamba yanayosimamiwa na serikali.
Sheria pia inawaruhusu wanaotumia bangi kupanda mimea yao nyumbani au kujiunga na vikundi vya sacco vinavyokuza mimea ya bangi.
Wauzaji wengi wa dawa hata hivyo wanasema wanashuku iwapo watapata faida yoyote ikiwa tayari bei yake imewekwa.
Baadhi ya wanunuzi pia hawakubaliani na amri ya serikali ya kuwasajili kwanza kabla kuwauzia bangi wakisema ni uvamizi wa hali yao ya faragha.
Vile vile hawakubaliani na pendekezo la kuwapimia kiwango cha bangi wanachonunua .
Tayari serikali imeandikisha mkataba na maduka 16 ya kuuza madawa na inatarajia kusajili maduka zaidi.
Roballo amesema kuwa kutakuwa na kampeni ya afya itakayofanywa kabla ya sajili kufunguliwa rasmi.
Alisema kuwa serikali kwa sasa haina uwezo wa kutosheleza mahitaji ya wanunuzi lakini haitarajii idadi yao kuwa kubwa zaidi.

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget