Articles by "Kitaifa"

Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH, Dokta Amos Nungu amesema taarifa ya utafiti huo haikuwafikia
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania ( COSTECH) imesikitishwa na kuvuja mitandaoni kwa mawasiliano ya barua iliyoiandikia Taasisi ya utafiti isiyo ya Kiserikali ya TWAWEZA.
Barua hiyo kuhusu kulitaka Twaweza litoe maelezo ndani ya siku saba kuhusu utafiti ulioifanya wa Sauti za Wananchi bila ya kibali, ambao umeonesha pia kushuka kwa uungaji mkono wa wananchi kwa wawakilishi waliowachagua.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa tume hiyo Dokta Amos Nungu amesema wameshangazwa kuona mawasiliano halali ya kiofisi yamesambazwa mitandaoni hata kabla ya kupata majibu rasmi.
Matokeo hayo ya utafiti, ndiyo yaliyoifanya Tume ya Sayansi na Teknolojia, ambayo ndiyo yenye jukumu la kuratibu, kufanya tathmini na ufuatiliaji wa tafiti, kuiandikia barua taasisi hiyo ya TWAWEZA, inayoonesha pia kwamba taasisi hiyo awali iliwasilisha maombi ya vibali vya kufanya utafiti nchini, lakini utafiti huo wa Sauti ya Wananchi haukujumuishwa.
Maelezo ndani ya barua hiyo imeitaka taasisi hiyo pia kutoa maelezo ndani ya ndani ya siku Saba.
'Mtafiti akija kutoa matokeo ya utafiti kwenye vyombo vya habari pia tunaona kuwa utafiti ulifanyika, huu utafiti tunakiri kuwa hatuna taarifa yake sababu mtafiti anaposajiliwa mwishoni anapoondoka na taarifa zake lazima ripoti ibaki COSTECH.Tumewaomba wiki moja watupe maelezo'' Dokta Amos Nungu, Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia.
Na kuhusiana na hatua gani watakazochukua juu ya mawasiliano hayo ya ndani kusambaa mitandaoni, amesema hilo ni jukumu la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
''tume inasikitika kuwa mawasiliano halali ya kiofisi yanapelekwa mitandaoni tumeziachia mamlaka kufanya kazi yake''.Alieleza Dokta Nungu
TWAWEZA imekiri kupokea barua kutoka COSTECH ''tumeipokea na tunaifanyia kazi. Twaweza haijasambaza, na haihusiki na usambazaji wa barua hiyo kwenye mitandao ya kijamii.
Barua yoyote inayofika Twaweza inagongwa muhuri wa kupokelewa mbele ya mjumbe aliyeleta barua hiyo. Barua inayosambaa mtandaoni hatuitambui kwa sababu haina muhuri wetu wa kuipokea Twaweza. Tunaheshimu na kuthamini sana mawasiliano yetu na wadau wetu''Alieleza Aida Eyakuze Mkurugenzi mtendaji wa TWAWEZA
source: https://www.bbc.com/swahili


Rais wa Tanzania John Magufuli leo hii ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa awamu ya kwanza ya mradi mkubwa wa reli ya kisasa ya Standard Gauge ambayo hapo baadae itaunganisha nchi za Rwanda na Burundi pia.
Lakini katika awamu hii ya kwanza, ujenzi utakuwa wa reli yenye urefu wa kilomita takribani 300, ambayo itatoka jijini Dar es Salaam na kuishia mkoa wa jirani wa Morogoro.
Ni reli ya kisasa, na ya kwanza Afrika Mashariki na kati itakayokuwa na uwezo wa kupitisha treni zitakazoendeshwa kwa nguvu ya umeme.
Reli hiyo itajengwa kwa awamu ya kwanza na kampuni kutoka nchi mbili, uturuki na Ureno kwa gharama ya takriban dola bilioni 1.2 za Kimarekani.
Reli hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba treni yenye kuvuta mabehewa 100 na kubeba mzigo wa mpaka tani 10000 kwa mkupuo sawa na uwezo wa Malori 500 ya mizigo.
Mradi huu utaleta ahueni kwa wasafiri wa Dar es Salaam mpaka Morogoro ambpo wataweza kusafiri kwa mwendo kasi kwa saa 2 na dakika 50 pekee
Rais wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli katika sherehe hizo amesema kuwa Tanzania itanufaika kutokana na Mradi huu kwa maendeleo ya uchumi,
Hivi sasa Serikali ya Tanzania inaelekeza jitihada zake za ujenzi wa reli wa awamu ya pili yenye urefu wa kilometa 336 kutoka Morogoro mpaka Dodoma yalipo makao makuu ya nchi na tayari serikali ya Uturuki imeonyesha nia ya kushirikiana na Tanzania kujenga sehemu hiyo.



Mwanamuziki Roma Mkatoliki amezungumza na waandishi wa habari leo kuhusu tukio la utekaji lililomkuta yeye pamoja na wenzake watatu usiku wa Jumatano wakiwa katika studio za Tongwe Records Masaki jijini Dar es Salaam.

Roma amesema kuwa walikuja watu waliokuwa na silaha za moto, wakawaamuru kuingia kwenye gari na kisha wakafungwa vitambaa usoni na pingu mkononi na kupelekwa eneo ambalo halijulikani. 

Wakiwa katika eneo hilo walihojiwa kwa siku tatu huku wakipigwa kabla ya kwenda kutupwa wakiwa wamefungwa katika eneo ambalo kwa haraka hawakujua ni wapi.

==>Haya ni baadhi ya Maneno ya Roma
1. Kwanza natoa shukrani kwa Mungu, kwenu, kwa wananchi na hasa wasanii wenzangu, nimeona mmesimama imara, pia serikali.

2.Kilichotokea ni kama case study maana kimetuunganisha wote bila kujali itikadi zetu, tuendelee kushikamana.

3.Niwaambie ukweli tu, mpaka sasa hatuna uhakika na usalama wetu, mahali tulipokuwa si pazuri kabisa.

4.Kama alifanyiwa daktari, baadaye akafanyiwa msanii, usishtuke kesho akafanyiwa mwandishi wa habari, au Mbunge.

5.Kinachotusikitisha zaidi ni maneno ya baadhi ya watu wanaodai kuwa tumepewa pesa ili tuitengeze hii, siyo sawa.

6.Ukweli ni kwamba tukio ni la kweli na tumepigwa sana, hadi sasa hatuko sawa kiafya.

7.Siku hiyo, walikuja watu wakiwa na silaha, na wamefunika nyuso zao, wakatuamrisha kuingia ndani ya gari.

8.Walitufunga macho na kutupeleka kusikojulikana, walitutesa sana, wametupiga sana.

9.Baada ya kupitia katika kipindi cha mateso makali, tuliachiwa usiku, tukaana kutembea bila kujua tuko wapi.

10.Siwezi kujua kama tukio hili linahusiana na muziki wangu, maana kuna hadi house boy wetu pia amehusika.

Hapo chini ni Video wakiongea


source:http://www.mpekuzihuru.com


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesikitishwa na vitendo walivyofanyiwa wasanii wa muziki Roma Mkatoliki na wenzake huku akisema hawezi kukubali kuona mambo kama hayo yakiwa yanaendelea kutokea.

Akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es Salaam, Waziri huyo amesema kilichotokea siyo hali ya kawaida kwa watanzania kamwe hawezi kukubaliana na jambo hilo huku akisisitiza kuwa atafuatilia kwa ukaribu sana ili aweze kupata majibu ya haraka kabla hajawasilisha bajeti ya wizara yake

"Hiki kilichotokea siyo hali ya kawaida kwa watanzania, hatuwezi kukubali kitu kama hiki kiendelee kutokea,nitalifuatilia kwa ukaribu sana, nitajitahidi nipate majibu kabla ya bajeti yangu Bungeni". Alisema Dk. Mwakyembe

Hata hivyo Dkt. Mwakyembe amewataka wananchi waache tabia ya kuamini kila maneno yanayosemwa na watu ambao hawana ujuzi katika masuala ya uchunguzi, hivyo wanapaswa kuvipa muda vyombo vya dola viweze kufanya kazi zake kwa ufasaha.

"Nilishasema kuwa nimeagiza vyombo vya dola vifanye uchunguzi ili ajulikane aliyewafanyia hivi wakina Roma kama ni nani kama wa dola ntadili naye, tuache uchunguzi ufanyike, tuache kupiga ramli". Alisisitiza Mwakyembe

Pia Waziri huyo mwenye dhamana na wasanii ametoa ujumbe kwa vyombo vyote vilivyopo chini ya Wizara yake kutofanya mahojiano yoyote yanayowahusu wasanii hao bila ya kuwepo taarifa kamili kutoka kwake.

Kwa upande mwingine Roma ambaye ambaye amesimulia tukio lilivyokuwa amesema kwa sasa hawezi kuongea mambo mengi kwa kuwa kila kitu amekwisharipoti polisi kila kitu, na kwamba kuna mambo akiyaweka hadharani atakuwa anaingilia upelelezi wa polisi.

Pia amesema hawezi kujua kama kweli tukio hilo lililowatokea  linahusiana na muziki kwa kuwa ameweza kuhusishwa mpaka mfanyakazi wao wa ndani ambaye hana hata chembechembe za uimbaji.

source:http://www.mpekuzihuru.com/2017/04/mwakyembe-ntahakikisha-nawapata.html

Image result for kamanda siro leo

Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Simon Sirro amesema kuwa tayari wameshapata taarifa za kupotea kwa Msanii wa Bongo Fleva hapa nchini, ‘Ibrahim Mussa’ maarufu kwa jina la Roma Mkatoliki na kuongeza kuwa tayari timu yake ya upelelezi imeshaanza kazi.

Ameyasema hayo mapema hii leo wakati akizungumza na Katibu wa Chama cha Wanamziki wa Kizazi Kipya Tanzania, Samweli Mbwana alipotaka kujua kama Jeshi la Polisi lina taarifa ya kupotea kwa mwanamziki huyo.

Sirro amesema kuwa taarifa za kupotea kwa msanii huyo tayari wameshazipata na Jalada la upelelezi tayari limeshafunguliwa kwa ajili ya upelelezi.

Ameongeza kuwa timu yake ya upelelezi iko mtaani kwa ajili ya kujua kinachoendelea, na amewaomba wasanii na baadhi ya watu kutokuwa wepesi wa kusambaza uvumi usiokuwa na ukweli ndani yake.

“Jamani mambo ya uvumi yaacheni, sio kitu kizuri unamvumishia mtu kitu ambacho hakijui na wengine wanasema kuwa Serikali inahusika kitu ambacho si cha kweli”,amesema Kamanda Sirro.

Aidha, Sirro amesema kuwa amepanga kukutana Waandishi wa Habari kesho saa tano Ofisini kwake ili kuweza kutoa ripoti kamili kuhusu kupotea kwa msanii huyo wa Bongo fleva kwani timu ya upelelezi tayari iko kazini.

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget