April 2017

http://www.cefc.com.hk/wp-content/uploads/2015/01/communication_sin300_37118315.jpg

Rais wa China Xi Jinping ametaka kuwepo uvumilivu kutoka pande zote wakati wa mawasiliano ya simu na rais wa Marekani Donald Trump siku moja baada ya Korea kusema kuwa ilikuwa tayari kuzamisha meli ya kubeba ndege za vita ya Marekani.
Mawasiliano hayo ya simu ndiyo ya pili kati ya viongozi hao wawili tangu wakutane huko Florida mapema mwezi huu.
Ni ishara ya hofu ya China kuwa msukosuko kati ya Marekani na Korea Kaskazini utasababisha mzozo.
Siku ya Jumapili vyombo vya habari nchini Korea Kaskazini vilisema kuwa jeshi la Korea Kaskazini lilikuwa tayari kuzamisha meli ya Marekani ya USS Carl Vinson, ambayo Marekani inasema itawasili katika rasi ya Korea siku chache zinazokuja.
Meli hiyo ilitumwa na Rais Trump huku onyo ikitolewa kuwa Marekani imepotza uvumilivu kwa mipango ya nuklia ya Korea Kaskazini.
Wakati wa mazungumzo hayo ya simu Bwana Xi alitaka pande zote kuwa wavumulivu na kuzuia vitendo ambavyo vimaweza kuzua mzozo.
Ikulu ya White House inasema kuwa bwana Trump amesisitiza kuwa vitendo vya Korea Kaskazini vinavuruga rasi wa Korea.
 Viongozi hao walikutana kati ya tarehe 7 na 8 huko Florida na baada kuzungumza kwa njia ya simu kuhusu Korea Kaskazni tarehe 12 mwezi Aprili.
source; bbc/swahili

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu anatarajiwa kuwa nje kwa miezi mitatu kutokana na maumivu ya goti la mguu wake kushoto. Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Eskilstuna nchini Sweden, Ulimwengu amesema kwamba amepokea taarifa za kusikitisha kutoka kwa Daktari wa timu yao.
"Juzi nilikwenda kupimwa na jana nikakutana na Daktari, maana nilivyoshitua goti kwenye mechi ya kirafiki nilianza maozezi ila bado ukawa unaendelea kuuma, hivyo jana ndiyo nimepewa hizi taarifa,"amesema Ulimwengu.Thomas Ulimwengu atakuwa nje kwa miezi mitatu kutokana na maumivu ya goti la mguu wake kushoto
Amesema ameambiwa anatakiwa kuwa nje kwa miezi mitatu kutokana na maumivu ya goti, baada ya vipimo alivyofanyiwa juzi nchini humo kufuatia kuumia Machi 23, akicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Malmo FF.Hakika huu ni mwanzo mbaya kwa Ulimwengu aliyejiunga na Eskilstuna Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Ulimwengu aliyezaliwa Juni 14, mwaka 1993 aliibukia katika taasisi ya soka Tanzania (TSA) mwaka 2008, kabla ya mwaka 2009 kwenda kuanza kukomazwa Ligi Kuu katika klabu ya Moro United alikokuwa akicheza kwa mkopo hadi mwaka 2010 alipokwenda akademi ya AFC Eskilstuna ya Sweden, alikocheza hadi mwaka 2011 alipochukuliwa na timu ya vijana ya Mazembe.
Alicheza U-20 ya Mazembe kwa msimu moja kabla ya kupandishwa rasmi timu ya wakubwa mwaka 2012 na moja kwa moja kuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza hadi anamaliza Mkataba wake Oktoba mwaka jana.Ulimwengu amehamia Ulaya baada ya kushinda mataji makubwa akiwa na Mazembe kama Ligi ya Mabingwa Afrika, Super Cup ya Afrika na pamoja na kucheza Klabu Bingwa ya Dunia.

Bingwa wa kutoa motisha afariki Afrika Kusini

Afrika Kusini inaomboleza kifo cha Ontlametse Phalatse, msichana wa umri wa miaka 18 ambaye alikuwa anaishi na ugojwa unaojulikana kama Progeria, ambayo ni hali ya kimaumbile isiyo ya kawaida ambayo husababisha mtu kuzeeka kwa haraka.
Mwezi uliopita Ontlametse alisherehekea siku ya kuzaliwa na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.
Seriklia ya Afrika kuisni imeongoza taifa kutuma rambi rambi kufuatia kifo hicho.
Alifariki hiyo jana katika hospitali ya Dr George Mukhari Academic iliyo nje ya mji wa Pretora.
Phalatse alikuwa mmoja wa wasichana wawili waliokuwa na hali hiyo nchini Afrika Kusini.
Alijiita "mama wa kwanza" , baada ya kuwa mtoto wa kwanza mweusi nchini Afrika Kusini, kupatikana akiwa na ugonjwa wa Progeria.
Alitajwa kuwa mtoto wa kuwapa watu motisha na mtot wa miujiza baada ya kuishi kuliko matarajio walioyokuwa nayo madaktari waliosema kuwa angefariki miaka minne iliyopita.
Rais Zuma ametuma rambi rambi zake kwa familia ya msichana huyo.
Bingwa wa kutoa motisha afariki Afrika Kusini
source:www.bbc.com/swahil

Rais wa Tanzania John Magufuli leo hii ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa awamu ya kwanza ya mradi mkubwa wa reli ya kisasa ya Standard Gauge ambayo hapo baadae itaunganisha nchi za Rwanda na Burundi pia.
Lakini katika awamu hii ya kwanza, ujenzi utakuwa wa reli yenye urefu wa kilomita takribani 300, ambayo itatoka jijini Dar es Salaam na kuishia mkoa wa jirani wa Morogoro.
Ni reli ya kisasa, na ya kwanza Afrika Mashariki na kati itakayokuwa na uwezo wa kupitisha treni zitakazoendeshwa kwa nguvu ya umeme.
Reli hiyo itajengwa kwa awamu ya kwanza na kampuni kutoka nchi mbili, uturuki na Ureno kwa gharama ya takriban dola bilioni 1.2 za Kimarekani.
Reli hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba treni yenye kuvuta mabehewa 100 na kubeba mzigo wa mpaka tani 10000 kwa mkupuo sawa na uwezo wa Malori 500 ya mizigo.
Mradi huu utaleta ahueni kwa wasafiri wa Dar es Salaam mpaka Morogoro ambpo wataweza kusafiri kwa mwendo kasi kwa saa 2 na dakika 50 pekee
Rais wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli katika sherehe hizo amesema kuwa Tanzania itanufaika kutokana na Mradi huu kwa maendeleo ya uchumi,
Hivi sasa Serikali ya Tanzania inaelekeza jitihada zake za ujenzi wa reli wa awamu ya pili yenye urefu wa kilometa 336 kutoka Morogoro mpaka Dodoma yalipo makao makuu ya nchi na tayari serikali ya Uturuki imeonyesha nia ya kushirikiana na Tanzania kujenga sehemu hiyo.



Simba wamepata ushindi wa kihistoria dhidi ya Mbao FC mechi ya ligi kuu Tanzania bara iliyochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.
Mbao FC walianza kwa kutangulia kupata magoli mawili kipindi cha kwanza na kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuibuka na pointi tatu katika mchezo huo. Magoli ya Mbao yamefungwa na Bernard dakika ya 18 na dakika ya 33.
Hadi dakika ya 80 Simba ilikuwa nyuma kwa magoli 2-0 matokeo ambayo kama yangebaki hivyo dakika 90 zinamalizika basi Wekundu wa Msimbazi wangekuwa kwenye nafasi finyu ya kutwaa taji la ligi kuu msimu huu.
Mabadiliko yaliyofanywa na benchi la ufundi la Simba kwa kumtoa Pastory Athanas na nafasi yake kuchuliwa na Said Ndemla, Blagnon na Mavugo wakaingia kuchukua nafasi za Liuzio na Hamad ndiyo yaliyo badili mchezo na kuipa Simba ushindi wa kwanza Kanda ya Ziwa msimu huu baada ya kuchapwa 2-1 na Kagera Sugar Jumapili iliyopita.
Magoli ya Simba yamefungwa dakika za lala salama ambapo goli lao la kwanza limefungwa dakika ya 82 na Frederick Blagnon. Uzembe wa golikipa wa Mbao Erick Ngwegwe ambaye aliuacha mpira udunde kisha akashindwa kuudaka kwa usahihi ulitua miguuni mwa Blagnon akafunga goli la pili dakika ya 90+1 na kufanya matokeo kuwa 2-2.
Wakati kila mmoja akiamini mchezo utamalizika kwa sare ya Mbao 2-2 Simba, Mzamiru Yassin akaifungia Simba goli la tatu dakika ya 90+7 kwa shuti kali baada ya beki wa Mbao kupiga kichwa mpira ambao ulitua kwa Mzamiru kisha kiungo huyo wa Simba kuachia mkwaju uliomshinda mlinda mlango wa Mbao.
Ushindi huo unaifanya Simba ifikishe pointi 58 ikiwa imecheza mechi 26 na kurejea kwenye nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kwa pointi mbili zaidi ya Yanga wanaoshuka kwenye nafasi ya pili lakini wakiwa na faida ya mechi moja mkononi.
Mbao inaendelea kubaki na pointi zake 27 ikiwa katika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi, pointi nne zaidi ya Toto Africans ambayo ipo katika timu tatu zitakazoshuka daraja.
Simba wataendelea kubaki jijini Mwanza wakisubiri kucheza dhidi ya Toto Africans timu ambayo imekuwa mwiba kwa ‘mnyama’ hususan mechi inapochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Mbao FC wamefungwa mechi zao zote (mbili) walizokutana na Simba msimu huu. Kabla ya kuchapwa 3-2 leo April 10, 2017, walifungwa 1-0 kwenye mchezo wa raundi ya kwanza uliochezwa October 20, 2016 kwenye uwanja wa Uhuru, Dar.
Swali ambalo mashabiki wengi wa Simba huenda wakawa hawajalipatia majibu ni kwanini Ibrahim Ajib, Laudit Mavugo, Said Ndemla na golikipa Daniel Agyei kuanzia nje wakati wanne hao wamekuwa wakifanya vizuri kwenye mechi za hivi karibuni?
Kikosi cha Simba kilichoanza kwenye mechi dhidi ya Mbao kiliongozwa na Juuko Murshid (nahodha), Peter Manyika Jr (GK), Hamadi Juma, Mohamed Hussein, Bessala Bokungu, James Kotei, Mzamiru Yassin, Juma Liuzio, Mohamed Ibrahim na Pastory Athanas.
Walionzia benchi ni Daniel Agyei, Mwinyi Kazimoto, Frederick Blagnon, Hija Ugando, Ibrahim Ajib, Said Ndemla na Laudit Mavugo.
source:www.shaffihdauda.co.tz


Mbunge wa Nzega Vijijini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Hussein Mohamed Bashe amesema kuwa ametumiwa ujumbe wa vitisho na watu wasiojulikana wakisema kuwa watamfanyika kitu kibaya popote pale alipo.

Bashe ambaye yupo kwenye vikao vya bunge vinavyoendelea mjini Dodoma ameandika leo asubuhi kupitia akaunti yake ya Tiwtter na Instagram  kuwa, ametumiwa ujumbe huo uliosomeka;

“Kuna watu wamenitumia ujumbe kwamba mimi ni kati ya watu 11 waliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale tulipo.

"Bunge na Serikali haiwezi kulifumbia macho jambo hili la Haramu wakati Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana. "

Kufuatia vitisho hivyo, Mbunge Hussein Bashe amelitaka Bunge na Serikali kutofumbia macho vitendo hivi vya wananchi kutekwa na watu wasiojulikana.



Mwanamuziki Roma Mkatoliki amezungumza na waandishi wa habari leo kuhusu tukio la utekaji lililomkuta yeye pamoja na wenzake watatu usiku wa Jumatano wakiwa katika studio za Tongwe Records Masaki jijini Dar es Salaam.

Roma amesema kuwa walikuja watu waliokuwa na silaha za moto, wakawaamuru kuingia kwenye gari na kisha wakafungwa vitambaa usoni na pingu mkononi na kupelekwa eneo ambalo halijulikani. 

Wakiwa katika eneo hilo walihojiwa kwa siku tatu huku wakipigwa kabla ya kwenda kutupwa wakiwa wamefungwa katika eneo ambalo kwa haraka hawakujua ni wapi.

==>Haya ni baadhi ya Maneno ya Roma
1. Kwanza natoa shukrani kwa Mungu, kwenu, kwa wananchi na hasa wasanii wenzangu, nimeona mmesimama imara, pia serikali.

2.Kilichotokea ni kama case study maana kimetuunganisha wote bila kujali itikadi zetu, tuendelee kushikamana.

3.Niwaambie ukweli tu, mpaka sasa hatuna uhakika na usalama wetu, mahali tulipokuwa si pazuri kabisa.

4.Kama alifanyiwa daktari, baadaye akafanyiwa msanii, usishtuke kesho akafanyiwa mwandishi wa habari, au Mbunge.

5.Kinachotusikitisha zaidi ni maneno ya baadhi ya watu wanaodai kuwa tumepewa pesa ili tuitengeze hii, siyo sawa.

6.Ukweli ni kwamba tukio ni la kweli na tumepigwa sana, hadi sasa hatuko sawa kiafya.

7.Siku hiyo, walikuja watu wakiwa na silaha, na wamefunika nyuso zao, wakatuamrisha kuingia ndani ya gari.

8.Walitufunga macho na kutupeleka kusikojulikana, walitutesa sana, wametupiga sana.

9.Baada ya kupitia katika kipindi cha mateso makali, tuliachiwa usiku, tukaana kutembea bila kujua tuko wapi.

10.Siwezi kujua kama tukio hili linahusiana na muziki wangu, maana kuna hadi house boy wetu pia amehusika.

Hapo chini ni Video wakiongea


source:http://www.mpekuzihuru.com


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesikitishwa na vitendo walivyofanyiwa wasanii wa muziki Roma Mkatoliki na wenzake huku akisema hawezi kukubali kuona mambo kama hayo yakiwa yanaendelea kutokea.

Akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es Salaam, Waziri huyo amesema kilichotokea siyo hali ya kawaida kwa watanzania kamwe hawezi kukubaliana na jambo hilo huku akisisitiza kuwa atafuatilia kwa ukaribu sana ili aweze kupata majibu ya haraka kabla hajawasilisha bajeti ya wizara yake

"Hiki kilichotokea siyo hali ya kawaida kwa watanzania, hatuwezi kukubali kitu kama hiki kiendelee kutokea,nitalifuatilia kwa ukaribu sana, nitajitahidi nipate majibu kabla ya bajeti yangu Bungeni". Alisema Dk. Mwakyembe

Hata hivyo Dkt. Mwakyembe amewataka wananchi waache tabia ya kuamini kila maneno yanayosemwa na watu ambao hawana ujuzi katika masuala ya uchunguzi, hivyo wanapaswa kuvipa muda vyombo vya dola viweze kufanya kazi zake kwa ufasaha.

"Nilishasema kuwa nimeagiza vyombo vya dola vifanye uchunguzi ili ajulikane aliyewafanyia hivi wakina Roma kama ni nani kama wa dola ntadili naye, tuache uchunguzi ufanyike, tuache kupiga ramli". Alisisitiza Mwakyembe

Pia Waziri huyo mwenye dhamana na wasanii ametoa ujumbe kwa vyombo vyote vilivyopo chini ya Wizara yake kutofanya mahojiano yoyote yanayowahusu wasanii hao bila ya kuwepo taarifa kamili kutoka kwake.

Kwa upande mwingine Roma ambaye ambaye amesimulia tukio lilivyokuwa amesema kwa sasa hawezi kuongea mambo mengi kwa kuwa kila kitu amekwisharipoti polisi kila kitu, na kwamba kuna mambo akiyaweka hadharani atakuwa anaingilia upelelezi wa polisi.

Pia amesema hawezi kujua kama kweli tukio hilo lililowatokea  linahusiana na muziki kwa kuwa ameweza kuhusishwa mpaka mfanyakazi wao wa ndani ambaye hana hata chembechembe za uimbaji.

source:http://www.mpekuzihuru.com/2017/04/mwakyembe-ntahakikisha-nawapata.html



Image result for hacking

Polisi nchini Uhispania wamemtia mbaroni mtaalam wa kompyuta kutoka Urusi kwa madai ya kudukua mitandao wakati wa uchaguzi marekani, habari kutoka vyombo vya habari vya Uhispania vimesema. Pyotr Levashov, ambaye alishikwa tarehe 7 Aprili, kwa sasa amewekwa rumande. Shirika la habari la AFP pia ilijulishwa kwamba Marekani ilikuwa imetoa ombi la Levashov kurudishwa nchini humo. Ombi hilo litapelelezwa na mahakama ya jinai ya Uhispania, AFP iliongezea. El Confidencial, tovuti ya habari Uhispania ilisema kuwa hati ya kukamatwa kwa Levashov ilitolewa na Marekani kwa kile kilichokisiwa kuwa kudukua mitandao hatua iliodaiwa kusaidia kampeni ya Trump.
source: http://www.bbc.com/swahili/habari-39558269

Image result for Nokia 3310

Kuna taarifa kwamba huenda simu muundo wa Nokia 3310 zikazinduliwa upya na kuanza kuuzwa tena .
Kampuni ya HMD Global Oy ya Finland, ambayo ina haki za kuunda bidhaa za nembo ya Nokia ndiyo inayodaiwa kuwa na mipango hiyo.Simu hizo inaarifiwa zitazinduliwa wakati wa Kongamano la Simu za Rununu Duniani baadaye mwezi huu.Kampuni ya Nokia ilinunuliwa na Microsoft mwaka 2013.Simu asilia za Nokia 3310 zilipata umaarufu kutokana na uthabiti wake.Nokia 3310/3330, zilizinduliwa 2000, na ni miongoni mwa simu zilizouzwa sana duniani. Jumla ya simu 126 milioni za aina hiyo zilitengenezwa na Nokia.
Kilicho ongezeka kwenye simu mpya za Nokia 3310.


sorce:bbc/swahili

Image result for kamanda siro leo

Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Simon Sirro amesema kuwa tayari wameshapata taarifa za kupotea kwa Msanii wa Bongo Fleva hapa nchini, ‘Ibrahim Mussa’ maarufu kwa jina la Roma Mkatoliki na kuongeza kuwa tayari timu yake ya upelelezi imeshaanza kazi.

Ameyasema hayo mapema hii leo wakati akizungumza na Katibu wa Chama cha Wanamziki wa Kizazi Kipya Tanzania, Samweli Mbwana alipotaka kujua kama Jeshi la Polisi lina taarifa ya kupotea kwa mwanamziki huyo.

Sirro amesema kuwa taarifa za kupotea kwa msanii huyo tayari wameshazipata na Jalada la upelelezi tayari limeshafunguliwa kwa ajili ya upelelezi.

Ameongeza kuwa timu yake ya upelelezi iko mtaani kwa ajili ya kujua kinachoendelea, na amewaomba wasanii na baadhi ya watu kutokuwa wepesi wa kusambaza uvumi usiokuwa na ukweli ndani yake.

“Jamani mambo ya uvumi yaacheni, sio kitu kizuri unamvumishia mtu kitu ambacho hakijui na wengine wanasema kuwa Serikali inahusika kitu ambacho si cha kweli”,amesema Kamanda Sirro.

Aidha, Sirro amesema kuwa amepanga kukutana Waandishi wa Habari kesho saa tano Ofisini kwake ili kuweza kutoa ripoti kamili kuhusu kupotea kwa msanii huyo wa Bongo fleva kwani timu ya upelelezi tayari iko kazini.

Image result for marijuana


Uruguay itaanza kuuza bangi kwenye maduka ya dawa kuanzia Julai.Nchi hiyo ya Marekani Kusini itakuwa ya kwanza duniani kuuza Bangi kihalali kwa matumizi ya kujiburudisha tu.
Safari ya kuhalalisha matumizi ya bangi ilianza mwaka wa 2013 baada ya sheria iliyokubali uuzaji na ununuzi wake kupitishwa.
Hata hivyo imechukua muda mrefu kwa sheria hiyo kuanza kutumika.
"Bangi itauzwa kwenye maduka ya dawa kuanzia Julai," msaidizi wa Rais, Juan Andre Roballo alisema katika kikao na wanahabari.
Sheria hii inawataka wanunuzi kujisajili na serikali. Bei yake itakuwa $1.30 kwa gramu moja.
Watakaojisajiliwa lazima wawe raia wa Uruguay au wakazi wa kudumu wa nchi hiyo na hawaruhusiwi kununua zaidi ya gramu 40 kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Marijuana hiyo itakuwa inapandwa kwenye mashamba yanayosimamiwa na serikali.
Sheria pia inawaruhusu wanaotumia bangi kupanda mimea yao nyumbani au kujiunga na vikundi vya sacco vinavyokuza mimea ya bangi.
Wauzaji wengi wa dawa hata hivyo wanasema wanashuku iwapo watapata faida yoyote ikiwa tayari bei yake imewekwa.
Baadhi ya wanunuzi pia hawakubaliani na amri ya serikali ya kuwasajili kwanza kabla kuwauzia bangi wakisema ni uvamizi wa hali yao ya faragha.
Vile vile hawakubaliani na pendekezo la kuwapimia kiwango cha bangi wanachonunua .
Tayari serikali imeandikisha mkataba na maduka 16 ya kuuza madawa na inatarajia kusajili maduka zaidi.
Roballo amesema kuwa kutakuwa na kampeni ya afya itakayofanywa kabla ya sajili kufunguliwa rasmi.
Alisema kuwa serikali kwa sasa haina uwezo wa kutosheleza mahitaji ya wanunuzi lakini haitarajii idadi yao kuwa kubwa zaidi.

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget