
Kuna taarifa kwamba huenda simu muundo wa Nokia 3310 zikazinduliwa upya na kuanza kuuzwa tena .
Kampuni ya HMD Global Oy ya Finland, ambayo ina haki za kuunda bidhaa za nembo ya Nokia ndiyo inayodaiwa kuwa na mipango hiyo.Simu hizo inaarifiwa zitazinduliwa wakati wa Kongamano la Simu za Rununu Duniani baadaye mwezi huu.Kampuni ya Nokia ilinunuliwa na Microsoft mwaka 2013.Simu asilia za Nokia 3310 zilipata umaarufu kutokana na uthabiti wake.Nokia 3310/3330, zilizinduliwa 2000, na ni miongoni mwa simu zilizouzwa sana duniani. Jumla ya simu 126 milioni za aina hiyo zilitengenezwa na Nokia.
Kilicho ongezeka kwenye simu mpya za Nokia 3310.
sorce:bbc/swahili
Kilicho ongezeka kwenye simu mpya za Nokia 3310.
sorce:bbc/swahili
Post a Comment